728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, May 16, 2016

    Kumbe Mikoani Kuna Mashabiki Zaidi Kayasema Bill Nas Hapa.


    Msanii Bill Nas amesema ziara yake ya mikoani anayoifanya imempa experience jinsi wanavyokubalika mikoani, lakini wao kama wasanii wanawasahau mashabiki wao wa mikoani.
     
    Bill Nas ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha  Vijana 101 kinachorushwa na Radio 101, na kuesema kuwa tofauti kubwa iliyopo kati ya miikoani na Dar ni kwamba Dar ni kama nyumbani na wamepazoea.

    “Experience kubwa ambayo nimeipata mikoani watu wanamiss vitu hivyo, kwa sababu Dar tuko hapa mara nyingi tunafanya, lakini pia watu wana love ya ukweli watu wameacha shughuli zao wanasema mi naishi hapa hapa (Dodoma) lakini ni mbali sana, mnapata pia nafasi ya kupata true fans, kuongea nao , kupiga picha, 

    pia unapata nafasi ya kukutana na artist wengine wa mikoani, kwa hiyo mikoani kuna vitu vingi sana na inatukumbusha kuwa hawa ndio watu wetu wanaotusapoti, iyo ndio kitu kikubwa ambayo mi nimeiona na tofauti kubwa kati ya Dar es salaam na mikoani.

    Bill Nas kwa sasa anaendelea na ziara yake ya kimuziki na kutangaza kazi zake zaidi, na hivi karibuni alikuwa mkoani Dodoma.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Kumbe Mikoani Kuna Mashabiki Zaidi Kayasema Bill Nas Hapa. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top