728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, May 22, 2016

    Uchunguzi wa ajali ya EgyptAir utachukua muda Mrefu Sababu Je?


    Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi, anasema kuwa kila kitu kinachoaminiwa kusababisa ajali, kinasalia jinsi kilivyo kuhusiana na ajali ya ndege ya EgyptAir, iliyoanguka siku ya Alhamisi.

    Bwana Al-Sisi amesema pia kuwa uchunguzi utachukua muda mrefu kukamilika huku akiviomba vyombo vya habari kujiepusha kueneza uvumi kuhusiana na kiini cha ajali hiyo.

    Hapo jana Jumamosi, wachunguzi wa Misri walisema ni mapema mno kufikia hatma ya kilichosababisha ajali hiyo kwani uchunguzi wa data bado haujakamilika.

    Kikosi kinachoendelea na msako kinaendelea kutafuta mabaki ya ndege hiyo pamoja na kisanduku cha kuhifadhi mawasiliano ya ndege.

    Ndege hiyo iliwauwa abiri wote 66 waliokuwemo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Uchunguzi wa ajali ya EgyptAir utachukua muda Mrefu Sababu Je? Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top