728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, May 23, 2016

    NAIBU WAZIRI ANELIJIBU SWALI LILILOMPONZA WAZIRI KITWANGA(video)..


    Yusufu amejibu upya swali lililomponza bosi wake wa  zamani, Charles Kitwanga. Uamuzi wa kurudia swali hilo ulitolewa juzi na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisema swali hilo lilijibiwa katika hali ya ulevi na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na wabunge wakaomba mwongozo kuhusu majibu yaliyotolewa.

    Kitwanga aliondolewa katika nafasi yake na Rais John Magufuli baada ya kujibu ya swali hilo akiwa amelewa.

    Leo, Masauni amejibu swali hilo namba 211 la Mbunge wa Viti Maalumu Devota Minja (Chadema) na kuonyesha utofauti mkubwa kati ya majibu yake na yale yaliyotolewa mwishoni kuongea kwa ulevi mwa wiki na aliyekuwa Waziri wake.

    Swali hilo ambalo awali lilikuwa namba 205, liliulizwa na Devota Minja akitaka kujua Serikali ina mpango gani wa kuboresha makazi ya polisi na askari magereza wanaoishi katika nyumba chakavu zisizokuwa na hadhi ukilinganisha na kazi zao kwa jamii.

    Nyakati zote hizo, swali hilo limeulizwa na wabunge tofauti wa Chadema kutokana na Minja kutokuwapo, mara ya kwanza likiulizwa na Suzan Kiwanga (Mlimba) na leo Joseph Selasini wa Jimbo la Rombo.

    Tofauti ya majibu ya Kitwanga, Masauni ametoa takwimu katika ujenzi wa nyumba 9,500 za Magereza nchi nzima, lakini kwa upande wa nyumba za Polisi majibu yalikuwa yaleyale.

    Tazama video ya majibu ya Naibu waziri hapa chini
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: NAIBU WAZIRI ANELIJIBU SWALI LILILOMPONZA WAZIRI KITWANGA(video).. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top