728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, May 18, 2016

    Amini: Sibaniwi ila nahisi muda wangu bado wa kutoboa.


    Msanii wa muziki wa Kizazi kipya Amini ‘Amini’ Mwinyimkuu, amesema hafikirii kama anabaniwa na wadau kwenye Tasnia ya muziki Bongo kama ambavyo imekuwa ikisemwa mara kwa mara, bali wakati wake wa kupewa heshima Zaidi bado haujafika.

    Akizungumza kupitia kipindi cha Jam Session cha Metro Fm ijumaa iliyopita, Amini amedai kila kitu ni wakati na subira katika kila kitu unachofanya.

    “Mwaka 2013 nilifanikiwa kupata tuzo basi unaambiwa wasanii wote walishangilia na kupanda juu ya meza, nafikiri muda wangu bado kila kitu kinahitaji subira, ipo siku tu ntatoa wimbo ambao Dunia nzima itaelewa nini nafanya” Alisema.

    Katika Hatua nyingine Amini ameweka bayana kuwa haamini kama mwanamuziki ukioa ndio Tiketi ya kupotea kwenye muziki kama wengi wanavyodai.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Amini: Sibaniwi ila nahisi muda wangu bado wa kutoboa. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top