Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Wales, Chris Coleman amemtema mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid katika kikosi cha wachezaji 29, kitakachoweka kambi nchini Ureno, kwa ajili ya maandalizi ya awali ya fainali za mataifa ya barani Ulaya (Euro 2016).
Coleman amechukua maamuzi ya kumtema mshambuliaji huyo, kutokana na
program zake kutomuhitaji kwa sasa, kufuatia jukumu zito linalomkabili
Bale katika klabu ya Real Madrid kwa sasa.
Bale anaendelea kuwa sehemu ya klabu hiyo ya mjini Madrid ambayo
inaendelea kupigania ubingwa wa nchini Hispania huku mchezo mmoja wa
ligi ya nchini humo ukisalia na FC Barcelona wakiwa kileleni kwa tofauti
ya point moja (88 kwa 87).
Mbali na jukumu hilo Bale ana anakabiliwa na mtihani mwingine wa
kujumuika na wenziwe huko mjini Madrid katika maandalizi ya kuelekea
kwenye mchezo wa hatua ya fainali wa ligi ya mabingwa barani Ulaya
ambapo Real Madrid watapambana na Atletico Madrid Mei 28 huko mjini
Milan nchini Italia.
Hata hivyo kocha mkuu wa Wales, anatarajiwa kumjumuisha Bale kikosini
mwake mwishoni mwa mwezi huu, ambapo atatangaza kikosi cha mwisho cha
wachezaji 23 ambacho kitaelekea nchini Ufaransa tayari kwa fainali za
mataifa ya barani Ulaya (Euro 2016).
Kikosi kilichotajwa na Chris Coleman kwa ajili ya kambi ya maandalizi
ya awali ya fainali hizo, upande wa makipa yupo Wayne
Hennessey, Danny Ward, Owain Fon Williams.
Mabeki: Ashley Williams, James Chester, Ben
Davies, James Collins, Chris Gunter, Adam Matthews,Neil Taylor, Adam
Henley, Paul Dummett, Ashley Richards.
Viungo: Joe Ledley, Joe Allen, David Vaughan, Emyr Huws, Jonathan Williams, David Edwards, George Williams, Aaron Ramsey, Andy King.
Washambuliaji: David Cotterill, Hal Robson-Kanu, Tom Lawrence, Simon Church, Sam Vokes, Wes Burns, Tom Bradshaw.
0 comments:
Post a Comment