Donald Trum Mgombea Nafasi ya Urais Nchini Marekani. |
Aliyekuwa
mgombea wa urais wa tiketi ya chama cha Republican nchini Marekani, Jeb
Bush amesema hatampigia kura Donald Trump katika Uchaguzi Mkuu
utakaofanyika nchini humo Novemba mwaka huu.
Bush alisema kuwa Trump hana tabia wala mienendo ya kuwa Rais wa Marekani.
‘‘Marais
wa Marekani wanasifa zao na wanakubalika kwa watu, lakini huyu jamaa
hana sifa hata moja ndiyo maana kila siku namkana na kusema hafai kabisa
kuwa rais wa nchi hii, ’’alisema Bush
Jeb
ni mojawapo wa wanachama mashuhuri wa Republican kutanganza hadharani
kuwa hatampigia kura Trump kwa sababu ya kampeni yake ya kiburi ambayo
imegawanya Chama cha Republican.
Juzi Spika wa Bunge, Paul Ryan alisema hatamuunga mkono mfanyabiashara huyo tajiri ingawa atakutana naye wiki ijayo.
Hata
hivyo, Trump aliungwa mkono na mgombea urais wa zamani wa nchi hiyo,
Bob Dole aliyeshindwa katika uchaguzi na Bill Clinton wa Chama cha
Democratic mwaka 1996.
Wiki
iliyopita Seneta wa Texas, Ted Cruz alijitoa katika kinyang’anyiro cha
kuwania uteuzi wa kugombea urais kwa Republican baada ya kushindwa
katika uchaguzi wa awali dhidi ya mpinzani wake huyo.
Cruz
aliwaambia wafuasi wake katika mji wa Indianapolis kwamba: “ Njia hii
kuelekea ushindi imefungwa” na kusema kuwa wapiga kura wamechagua njia
nyingine.
Alitoa
shukrani kwa wafuasi wake wote. Trump alipata ushindi mkubwa Indiana
huku Cruz akishika nafasi ya pili na gavana wa Ohio John Kasich akiwa
katika nafasi ya tatu.
Trump
alisema huo ni ushindi mkubwa kwake na kumpongeza Cruz akimuita yeye na
wagombea wengine 15 waliokuwa wanagombea uteuzi wa Republican kuwa ni
werevu na wenye nguvu.Alitoa wito wa kuwa na umoja ndani ya chama hicho.
Kwa upande wa Democratic seneta wa Vermond, Bernie Sanders ameshinda katika jimbo la Indiana dhidi ya Hillary Clinton
Wagombea
hao wawili walibadilishana ushindi kabla ya Sanders kuibuka mshindi kwa
asilimia saba ya kura. Hata baada ya ushindi huo wa Sanders katika
jimbo la Indiana, Hillary anaongoza katika idadi ya wajumbe ikionyesha
kwa mahesabu ni vigumu kwa Sanders kuteuliwa kuwa mgombea wa Democratic
0 comments:
Post a Comment