Baadhi ya mashabiki waliokua wamejikusanya makao makuu ya klabu ya Simba mtaa wa msimbazi jijini Dar es salaam. |
Mashabiki wa klabu ya Simba SC wameandamana na kuvamia makao makuu ya
klabu eneo la Msimbazi mapema leo asubuhi kuushinikiza uongozi uachie
ngazi kwa madai kwamba wameshindwa kuisimamia timu yao.
Mashabiki hao wenye hasira wameamua kukusanyika kufuatia matokeo ya
kufungwa katika na timu ya Mwadui FC katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa
jana katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam, na kuiacha Simba
katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wakitanguliwa na Azam FC
walioshinda jana kwenye mechi yao dhidi ya Kagera Sugar.
Jambo lingine lililowapandisha hasira mashabiki hao ni kauli kali
aliyoitoa kocha wa Mwadui FC, Jamhuri Kiwelo Julio ambaye amewahi
kucheza kwenye klabu hiyo miaka ya nyuma na pia kuwa kocha msaidizi
kabla ya kutimuliwa yeye na mwenzake Abdallah Kibaden.
Julio alisikika akisema kuwa kitendo cha Simba kufanya vibaya ni
laana yake yeye na Kibaden ambao walifukuzwa Simba kihuni na kuletwa
kocha Mzungu ambaye hata hivyo naye alifukuzwa baada ya kushindwa
kuonesha kile uongozi ulichokuwa unakitaka.
‘Simba ni kama muembe wangu wa uani najiokotea tu dodo ninavyotaka,
na siku zote nasema hii ni laana kwa sababu haiwezekani sisi tufukuzwe
bila sababu ya msingi halafu aletwe kocha mwingine eti kwa kuwa ni
mzungu na cha kushangaza sisi tuliiacha Simba ikiwa katika nafasi ya
tatu huyo mzungu wao amemaliza ligi Simba ikiwa katika nafasi ya nne,
sasa nani bora? Alisema Julio.
Julio amesema kitendo cha kufukuzwa bila kufuata taratibu za
makubaliano kimewauama na kitaendelea kuwauma lakini wamemuachia
mwenyezi mungu na ndiyo maana laana inawarudia wenyewe.
0 comments:
Post a Comment