Wilaya Uyui Mkoani Tabora inatarajia kuanza kampeni ya kuondoa nyumba zote za tope,ili kuwanusuru wananchi na maafa kama yaliyotokea wakati wa mvua za masika kati ya mwezi Februari hadi Aprili mwaka huu.
Akizungumza
kwenye baraza la Madiwani Mkuu wa Wilaya hiyo, Zuhura Mustapha Ally,
amesema kampeni hiyo inaanza mapema mwezi huu baada ya mvua za masika
kukatika na kusema zoezi hilo litawagusa waliobomokewa na nyumba zao na
wale wenye nyumba za udongo.
Mkuu huyo wa Wilaya amewaomba madiwani wa Halmashauri hiyo kushirikiana na serikali katika kampeni hiyo, ambayo inamtaka kila mwananchi kujenga nyumba ya tofali za kuchoma.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri, amesema ujenzi wa Nyumba bora unategemea vipato vya ziada vya wananchi hivyo amewataka wananchi kuuza ziada ya mazao yao na kuwaomba Madiwani na Watendaji wa Kata na Serikali ya Vijiji kusimamia zoezi hilo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Uyui, Dkt. Said Mtahondi, amesema kuwa hivi sasa kero kubwa ya wananchi wake ni malipo ya pili ya tumbaku yao.

0 comments:
Post a Comment