Washika bunduki wa kaskazini mwa jijini London (Arsenal), wametenga
kiasi cha Pauni million 34, kwa ajili ya usajili wa kiungo kutoka
nchini Uswiz pamoja na klabu ya Borussia Monchengladbach ya nchini
Ujerumani, Granit Xhaka.
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amehusishwa kwa muda mrefu na
taratibu za usajili wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23, na kwa sasa
anaamini huenda akampata kutokana na fungu la pesa alilolitenga.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti la The Sun la nchini England, umebaini
kwamba, meneja huyo kutoka nchini Ufaransa amedhamiria kumsajili kiungo
huyo kabla ya kujiunga na kikosi cha timu ya taifa ya Uswiz, ambacho
kitaelekea nchini Ufaransa kushiriki fainali za mataifa ya barani Ulaya
(Euro 2016).
Nguvu ya usajili wa Granit Xhaka, inahisiwa kuongezeka miongoni mwa
maafisa wa Arsenal wakiongozwa wa Arsene Wenger, kufuatia uongozi wa
klabu ya Borussia Monchengladbach, kushindwa kumshawishi abaki kwa
kipindi kingine.
Hata hivyo hapo awali ada ya uhamisho wa Xhaka, ilitajwa kuwa Pauni
million19.7, lakini kutokana na uwepo wa klabu kadhaa ambazo zinaiwania
saini yake, mchezaji huyo amepandishwa thamani na kufikia zaidi ya Pauni
million 25.
Arsene wenger amejipanga kuiboresha safu yake ya kiungo, kufuatia
baadhi ya wachezaji wake waliopo kikosini kwa sasa wanaocheza nafasi
hiyo kumaliza mikataba yao kama Mathew Flamini, Tomas Rosicky pamoja na
Mikael Arteta.
0 comments:
Post a Comment