KOCHA mkuu wa Mbeya City Fc, Kinnah Phiri muda mfupi uliopita
ametangaza kikosi cha nyota 11 watakaoanza kwenye mchezo wa leo dhidi
ya Yanga katika kinyang’anyiro cha ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Katika kikosi hicho mlinda mlango Juma Kaseja anaendelea kusimama
langoni sambamba na walinzi wa kulia na kushoto, John Kabanda na Hassan
Mwasapili.
Wengine katika kikosi hichi ni kama ifuatavyo.
1.Juma Kaseja 2. John Kabanda 3. Hassan Mwasapili 4. Tumba
Lui 5.Haruna Shamte 6.Kenny Ally 7. Seleman Mangoma 8. Ramadhan Chombo
9. Salvatory Nkulula .10 Geoffrey Mlawa 11 Joseph Mahundi
SUB: Hanningtony Kalyesubula, Hamidu Mohamed, John Jerome,Ditram Nchimbi,Haruna Moshi,Raphael Daud na Yohana Moriss.
Mchezo huu namba 218 umepangwa kuanza saa 10:00 na utachezeshwa na
mwamuzi Jimmy Fanuel kutoka Shinyanga, huku kiingilio kwa mashabiki
kikiwa ni shilingi 5000 tu.
Haijawahi kutokea hapo
kabla! Bendi kumi na moja za taarab kuumana kwenye jukwaa moja na
kukumbuka taarab ilipotokea, ni tukio la kwanza litakalotokea mwezi huu
tarehe 21.
Hiyo itakuwa ndani ya ukumbi wa Dar Live ambapo show maalum iliyopewa
jina la “Usiku wa ya kale ni dhahabu” itanguruma kuanzia saa 1 za usiku.
Mratibu wa onyesho hilo, Juma Mbizo, ameiambia Saluti5 kuwa siku siku
hiyo zitapigwa nyimbo zote kali za taarab zilizotamba katika ya miaka ya
90 na 2000.
Mbizo amesema bendi zitakazokuwepo Dar Live siku hiyo ya Mei 21 ni
Mamesh, All Star, Alwatan, TOT Taarab, Muungano, JKT Taarab, na Babloom
Modern Taarab.
Bendi zingine zitakazokuwepo kwa mujibu wa Mbizo ni Egyption, East
African Melody, Zanzibar Stars na Jahazi Modern Taarab.
“Hapo kabla, halijawahi kufanyika onyesho kama hili, hii ni mara ya
kwanza katika historia ya muziki wa taraab,” alisema Juma Mbizo.
Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2016/05/usiku-wa-ya-kale-ni-dhahabu-kuandika.html
Copyright © saluti5
Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2016/05/usiku-wa-ya-kale-ni-dhahabu-kuandika.html
Copyright © saluti5
0 comments:
Post a Comment