Msanii wa muziki wa Bongo flava, Harmonize, ameweka wazi kuwa pesa zilizotumika kununua gari yake ya kwanza mpya aina ya Mark X hazijatokana asilimia 100 na shows alizopiga mpaka sasa.
Kwenye Exclusive na kipindi cha Vijana101, Star huyo mmiliki wa Hit single ya ‘Bado’, amedai kuwa uongozi wake wa WCB
umeona kuwa kwa kiwango alichofikia hivi sasa anahitaji kumiliki usafiri
wake yeye mwenyewe.
“Lakini hii gari haijatokana na shows zangu, management yangu imeona
kwa hatua niliyofikia kwa sasa nahitaji kuwa na usafiri wangu ili kutoa
morali pia kwa vijana wengine wanaochipukia kimuziki,.
“Nyimbo zangu zinafanya vizuri si haba ni gari nzuri ambayo kila mtu anandoto ya kuwa nayo” Alisema.
0 comments:
Post a Comment