Klabu za jijini London nchini England, Chelsea na Arsenal zimeanza
kuonyesha makeke ya kuihitaji saini ya kiungo wa mabingwa wa soka wa
EPL, Leicestter City, N’golo Kante.
Chelsea na Arsenal zimekua za kwanza kuonyesha makeke ya kumuwania
kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25, kutokana na hamasa ambazo zimeanza
kuchukua nafasi ndani kwa ndani kwenye makao makuu ya klabu hizo.
Ushujaa na kujituma kwa Kante katika kipindi chote cha msimu wa
2015-16, kumekua chagizo la klabu hizo mbili kufikiria namna ya
kumsajili mara baada ya dirisha litakapofunguliwa siku kadhaa zijazo.
Hata hivyo tayari kuiungo huyo kutoka nchini Ufaransa,
ameshatahadharishwa na meneja wa Leicestter City, Claudio Ranieri juu ya
kutokufanya maamuzi ya kusaka mahala pengine pa kucheza msimu ujao na
badala yake afikirie kubaki King Power Stadium.
Mbali na klabu hizo za jijini London, pia mabingwa wa soka nchini
Ufaransa Paris Saint Germain (PSG) nao wamejitangaza hadharani kumuwania
Kante huku wakiamini kiasi cha Pauni million 19.7 kitatocha kuvunja
mkataba wake.
Kante ambaye anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya
Ufaransa ambacho kitashiriki fainali za mataifa ya barani Ulaya (Euro
2016) mwezi ujao, amekua akilipwa mshahara wa Pauni elfu 25 (25,000) kwa
juma tangu alipojiunga na Leicester City mwanzoni mwa msimu huu.
Udhaifu huo wa malipo umebainiwa na viongozi wa klabu hiyo na sasa
wanajipanga kumuandalia mkataba mpya ambao utamuwezesha kulipwa vizuri.
Kigezo cha mshahara wake kimekua kikitajwa kama sehemu ya
kuzishawishi klabu nyingine kumuwania kwa urahisi Kante katika kipindi
hiki cha kuelekea mwishoni mwa msimu huu.
0 comments:
Post a Comment