Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na michezo kwa kushirikiana na
vyombo vingine vinavyoshughulika na sanaa ikiwemo BASATA wamekubaliana
kuufungia wimbo na video ya Chura kupigwa kwenye vyombo vya Habari,
maeneo ya hadhara na mahala popote kwenye mkusanyiko wa watu.
Serikali kupitia muwakilishi wake imedai kuwa, wimbo huo unadhalilisha na kukiuka haki za binadamu.
Wizara pia imebaini kuwa Msanii Snura, hana nyaraka maalum za
kujihusisha kwenye masuala ya muziki, hivyo imemfungia kujihusisha na
matamasha ya aina yoyote mpaka pale atakapotimiza taratibu.
Msanii huyo ameamriwa kutoa haraka video hiyo kwenye mitandao ya
kijamii ikiwemo Youtube, na kwa mtu yoyote atakayeisambaza kwenye
mitandao ya kijamii atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Kama ulikosa itazame hapa chini Video ya snura iliyofungiwa hapa chini.
Kama ulikosa itazame hapa chini Video ya snura iliyofungiwa hapa chini.
0 comments:
Post a Comment