Mchezaji wa timu ya Real Madrid, Cristiano Roanaldo ameuomba uongozi wa
Madrid wasimuachie kocha wa timu hiyo Zinedine Zidane aondoke msimu
ujao.
Zidane ambaye alichukuwa mikoba ya kuifundisha timu hiyo mwezi
Januari kutoka kwa Rafael Benitez ambaye kwa sasa anaifundisha timu ya
Newcastel United ya nchini Uingereza.
Tangu Zidane aanze kuifundisha timu ya Real Madrid wamefanikiwa
kucheza michezo 23 na kushinda michezo 18 na kuanza kuiweka timu hiyo
kwenye nafasi nzuri ya kuwania ubingwa wa La Liga wakiwa nyuma ya pointi
mbili na vinara wa ligi hiyo, Barcelona na Atletico Madrid wenye pointi
sawa.
Ronaldo amesema, “Nadhani tunahisi kuwa na furaha zaidi chini ya
Zidane. Tunahisi upendo wake, tunajua kwamba yupo katika kipindi cha
kuzoea mazingira, lakini mambo yamemnyookea kwa haraka sana name
namfurahia pia.”
“Daima nilivutiwa naye kama mchezaji, na sasa ni kocha hali
kadhalika, jinsi anavyofanya mambo yake na kushughulika na wachezaji.
Jinsi anavyofundisha tu ningependa aendelee kubaki Real Madrid,”
aliongezea Ronaldo.
Ronaldo ambaye amekuwa nje ya uwanja kwa takribani michezo mitatu
kutokana na kuwa majeruhi anatarajiwa kuwepo uwanjani kwenye mchezo wa
marudioano wa Uefa kati ya Madrid dhidi ya Manchester City ambao
utafanyika kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu siku ya Jumatano.
0 comments:
Post a Comment