Msanii wa muziki kutoka Tip Top Connection, Madee amefunguka na kudai
kuwa siku zote atamlaumu msanii wa Bongo flava na aliyewahi kuwa chini
ya usimamizi wa Tip Top, Mb Doggy kwa kuondoka kwenye lebo hiyo.
Akizungumza katika kipindi cha Hatua Tatu cha Times Fm, Madee amedai
Mb Dog alikosea kuondoka Tip Top kwa kuwa alikuwa chini ya mikono
sahihi.
“Mimi kitu ambacho nitaendelea kumlaumu Mb Doggy ni kuondoka Tip Top,
unajua unapokuwa kwenye malezi ya baba na mama mmoja hata maadili ni
yale yale, unapoenda sehemu nyingine unakutana na vitu vipya, alafu si
tulikuwa tukitoa nyimbo Babu tale ndiyo anaenda kushughulika kila kitu
kupeleka Radio na vitu vingine, sasa hakuwa na menejimenti kila kitu
alikuwa akifanya yeye baada ya kutoka nahisi ndiyo maana akashindwa”
Alisema.
Kwa sasa MB Dog yupo chini ya label ya QS Mhonda Entertainment pamoja
na Q Chief. Ambapo mpaka sasa ameshaachia kazi kadhaa, moja wapo ni
video ya wimbo ‘Sio Siri’ ambayo ulifanya vizuri.
0 comments:
Post a Comment