728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, May 6, 2016

    Pambana achana na mambo yasiyo na msingi Kijana fanya hivi ili kufanikisha mambo yako.Ray anamajibu hapa.


    Msanii wa filamu nchini Ray Kigosi amefunguka na kusema kuwa yeye furaha yake ni kuona vijana wenzake wakifanikiwa na kupiga hatua kimaendeleo.

    Kwenye Exclusive interview na Vijana101 Radio show, Ray Kigosi amewaasa vijana wenzake kuwa wasikae wakategemea kuwa viongozi wa siasa wanaweza kuja kuwabadilishia maisha yao bali amewataka kuwa na jitihada binafsi kwani huo ndiyo msingi mkubwa wa mustakabali wa maisha yao.


    “Furaha yangu ni kuona kijana mwenzangu ukifanikiwa na kupiga hatua kimaendeleo, pambana achana na mambo yasiyo na msingi ukitaka kufanikiwa katika ndoto zako fanya vitu vigumu kufanyika. 

    Fanya kitu ambacho mwingine hawezi kufanya, hakuna kiongozi yeyote wa nchi atakayekuja kuyabadilisha maisha yako isipokuwa ni jitihada zako mwenyewe huo ndio msingi mkubwa wa mustakabali wa maisha yako.”
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Pambana achana na mambo yasiyo na msingi Kijana fanya hivi ili kufanikisha mambo yako.Ray anamajibu hapa. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top