Mshambuliaji kutoka nchini England na klabu ya Arsenal, Theo Walcott
yuko njiani kuondoka kaskazini mwa jijini London na kuhamia magharibi mwa
jiji hilo yalipo makao makuu ya klabu ya West Ham Utd.
Walcott yuko tayari kuachana na Arsenal, mwishoni mwa msimu huu, baada
ya kuchoshwa na mpango wa meneja wa klabu hiyo Arsene Wenger wa kumtumia
kama mchezaji wa akiba.
Tayari amzungumzo ya awali kati ya mchezaji huyo na uongozi wa The
Gunners yameshafanyika juu ya kutarajia kuondoka kwake mwishoni mwa
msimu huu, na sasa kinachosubiriwa ni kutumwa kwa ofa ya klabu ambayo
itakuwa tayari kumsajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27.
Klabu ya West Ham Utd, imekua ya kwanza kuonyesha nia ya dhati ya
kutaka kumsajili Walcott, kufuatia mipango iliyowekwa hadharani na
wawekezaji klabuni hapo David Gold na David Sullivan ya kuandaa ofa ya
kufanya usajiali wa mshambuliaji mwenye uzoefu na ligi ya nchini
England, kama walivyoagizwa na meneja wao Slaven Bilic.
Uongozi wa klabu hiyo unaamini Walcott, ni mchezaji mwenye vigezo
vinavyotakiwa na meneja huyo kutoka nchini Croatia, na atakapowasili
huko magharibi mwa jijini London atawasidia kufikia lengo la kufanya
vizuri zaidi, tofauti na ilivyokua msimu huu.
West Ham Utd, pia imeonyesha nia ya kutaka kumsajili kiungo wa klabu
ya Olympic Marseille Michy Batshuayi pamoja na mshambuliaji wa klabu ya
Olympic Lyon Alexandre Lacazette.
Pia yupo mshambuliaji wa klabu ya Inter Milan, Mauro Icardi ambaye pia anawaniwa na klabu za Man Utd pamoja na Chelsea.
0 comments:
Post a Comment