Mwimbaji
wa muziki wa Mduara nchini Snura Mushi ameomba radhi kwa umma wa
Watanzania kwa kosa la kutengeneza, kuzindua na kuweka mitandaoni video
ya udhalilishaji wa mwanamke na isiyozingatia maadili ya Kitanzania ya
muziki unaoitwa "Chura"
Akizungumza na vyombo vya habari leo Snura amesema wakati wa utayarishaji wa video hiyo mvua ilinyesha hivyo madansa walilowana.
"Baada
ya kuona wamelowa ilibidi tusitishe kupeleka katika televisheni na
kuiacha you tube, Snura hajafungiwa bali video yangu ilisitishwa na mimi
nilizuiwa kujihusisha na sanaa mpaka nijisajili," amesema Snura.
Meneja
wa mwanamuziki huyo Hemedi Kavu amesema tayari walishakwenda Basata
tangu jana kuomba usajili, leo wamepatiwa cheti cha usajili.
"tumeshajisajili
Basata, pia tayari tumeshaitoa video hiyo kwenye mtandao wa YouTube,
tumeshalitekeleza na akaunti ya wimbo huo imeshafutwa na tunatarajia
kuifanya video hiyo upya," amesema Hemedi Kavu.
0 comments:
Post a Comment