Kocha mkuu wa
klabu ya Mwadui FC ya mkoani Shinyanga, Jamhuri Kiwelu Julio, amewatolea uvivu
viongozi wa klabu ya Simba chini ya mwenyekiti wake Evans Aveva, kwamba
wamekalia majungu na roho mbaya ndani ya klabu hiyo na ndiyo sababu ya
kushindwa kufanya vizuri kwa msimu wa nne sasa.
Amesema kipindi
ambacho walikuwa wanakinoa kikosi cha Simba akiwa chini ya Abdallaha King
Kibaden kama kocha msaidizi, kulikuwa na ukiritimba mkubwa ndani ya klabu hiyo
kiasi cha kufikia hatua ya kuwatimua wakati timu ikishikilia nafasi ya tatu kwa
madai kwamba hawana msaada wowote.
Itakumbukwa kwamba
baada ya Julio na Kibaden kutimuliwa Simba ikiwa inashikilia nafasi ya tatu,
uongozi ukafanya makubaliano na kumleta kocha wa kigeni Logarusic, ambaye
alikiongoza kikosi hicho hadi mwishoni mwa msimu na kumaliza wakiwa katika
nafasi ya nne.
“Ubabaishaji, roho
mbaya na ukiritimba uliopo ndani ya Simba utawafanya wazidi kuweweseka kila
msimu, wewe angalkia mimi na Kibadeni walitufukuza kihuni bila hata kutulipa
stahiki zetu,”
“Wakamuajiri kocha
mzungu ambaye amekuja kula tu hela zao lakini hakuna chochote alichofanya,
tumeiacha timu ikiwa katika nafasi ya tatu yeye kawaporomosha hadi nafasi ya
nne” Alisema Julio.
Klabu hiyo kongwe
nchini inamaliza msimu wa nne sasa bila kuchukua ubingwa licha ya kubadilisha
makocha kadhaa wa ndani na wale wa kigeni.
0 comments:
Post a Comment