Klabu ya Ruvu Shooting ipo kwenye mchakato wa usajili ila imeweka
wazi kuwa wachezaji kutoka timu za Simba na Yanga wasahau kuichezea timu
hiyo kwani hawana uvumilivu na hawajitumi.
Ruvu Shooting imepanda kushiriki Ligi Kuu Bara msimu ujao na bado inaendelea kufundishwa na Tom Olaba ambaye ni Kocha Mkuu.
Msemaji wa Klabu hiyo, Masau Bwire, alisema hawawezi kusajili
wachezaji kutoka timu hizo kongwe kwani licha ya kutocheza kwa kujituma
pia nidhamu zao ni mbovu.
“Hatuna mpango wa kusajili makapi ya Simba na Yanga kwani wachezaji
hao huwa mara nyingi hawana moyo wa kupambana na pia nidhamu zao ni
mbovu,” alisema Masau.
Alisema kocha wao mkuu, Olaba amependekeza kikosi chao kusajili
wachezaji saba wenye vipaji ambapo uongozi unalifanyia kazi jambo hilo
ili kutimiza matakwa yao ya kuwa na timu imara msimu ujao.
0 comments:
Post a Comment