728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, May 4, 2016

    Nando amesema anajuta kushiriki Big Brother, akili kuwahi kutumia Madawa ya kulevya aliyoacha miaka 2 iliyopita, vipi kuhusu Bangi? itakushangaza.

    Mshiriki wa shindano la Big Brother Africa mwaka 2013 kutokea Tanzania, Amiry Nando, amesema katika mambo anayojutia katika maisha yake ni kujiunga katika kinyang’anyiro cha Big Brother.

    Kwenye Exclusive interview na Metro fm jana  Star huyo mwenye vituko na Mbwembwe nyingi amedai hakuna alichokivuna BBA zaidi ya hasara na umaarufu usio na faida.

    “Hakuna faida yoyote niliyoipata BBA, najuta sana kushiriki aisee zaidi ya watu kuja kukusahangaa bila mpango hakuna faida yoyote” Alisema.

    Katika hatua nyingine Nando amezungumzia tetesi za yeye kutumia Madawa ya kulevya, na nini hasa kinasababisha vijana kuloea katika matumizi hayo yasiyo na faida.

    “Mimi nilikuwa natumia ‘Cocaine’ lakini nimeacha tangu 2014, kwa sasa labda fegi (sigara) na Ganja (Bangi) tu, unajua kinachowafanya wakina Chid kuwa mateja ni kwamba wao wanavuta kwahiyo inaathari kubwa kuliko kusnifu, we njoo mbudia pale utaona mi natumia Ganja tu alafu naenda na chips mayai zangu mbili nini” alieleza.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Nando amesema anajuta kushiriki Big Brother, akili kuwahi kutumia Madawa ya kulevya aliyoacha miaka 2 iliyopita, vipi kuhusu Bangi? itakushangaza. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top